Kimbunga
|
| Price: |
ONLY 8 AVAILABLE! Swahili poetry from Zanzibar.
Kimbunga, katika lugha ya kawaida, ni neno linaloashiria dhana ya tufani kali liwezalo kuvunja nyumba, kuezua vipaa na kusabibisha maafa ya namna kwa namna. Katika tungo hizi za Bwana Haji Gora Haji, Kimbunga ni fumbo. Badala ya kuathiri kila kitu kutokana na nguvu zake, chenyewe kuathiri baadhi tu ya vitu na vyengine hunusurika. Mbuyu unapong'olewa na mnazi kunusurika; majabali yanapobirukizwabirukizwa, meli zikadidimia na ngarawa kuokoka; magorofa yakarushwa angani na vibanda vikasalimika tunahisi kuwa hiki si kimbunga cha kawaida.
Mtunzi wa mashairi haya Bwana Haji Gora Haji, alizaliwa katika kijiji cha Kokoni, Tumbatu, Zanzibar, mwaka 1933. Bwana Haji Gora Haji hakubahatika kwenda shule, bali alijielimisha mwenyewe hadi akawa mtunzi mahiri wa nyimbo na mashairi. Kazi alizopota kuzifanya ni uvuvi, ubaharia na ukuli. Hivi leo mshairi huyu anaishi Chumbuni, wilaya ya mjini Zanzibar, na anafanya kazi ya Uchukuzi.

Product Description
Tungo za Visiwani - Swahili Poetry
Product Details
- Amazon Sales Rank: #7335783 in Books
- Published on: 1994
- Binding: Paperback